MAT Leadership application announcement

TANGAZO LA UCHAGUZI

Chama cha Madaktari Tanzania (MAT) kinatarajia kufanya uchaguzi wa viongozi wa kukiongoza chama kwa miaka miwili ijayo.

Kwa tangazo hili, wanachama wote hai wa MAT wanakumbushwa kuhudhuria mkutano mkuu wa chama utakao fanyika sambamba na Kongamano la 50 la afya, tarehe 24 hadi 26 Oktoba mwaka huu.

Kwa wale wenye nia ya kugombea, watajaza fomu maalumu siku ya kwanza ya Kongamano. Hii itafuatiwa na uchaguzi wa viongozi utakaofanyika siku ya pili ya mkutano mkuu wa chama.

Nafasi ziitakavyogombewa ni pamoja;

1. Rais mteule (President Elect)

2. Katibu na Katibu Msaidizi

3. Muweka Hazina na Muweka Hazina Msaidizi

4. Wanachama saba wa Baraza la uongozi MAT

Imetolewa na Katibu mkuu wa Chama cha Madaktari Tanzania (MAT).